Africa:
Hatua ya Kwanza ya Kuokoa Misitu ya Burkina Faso

Reprint | | Print |

OUAGADOUGOU - Burkina Faso imepata msaada wa dola milioni 30 kutoka Mpango wa Uwekezaji Katika Misitu (FIP) kusaidia kutunza misitu ya nchini humo na kupunguza hewa ukaa inayotokana na kuteketezwa kwa misitu.
 
Mpango wa FIP utafanya kazi katika mikoa minne ya nchi hiyo, kila mkoa ukiwakilisha bayoanuwai tofauti. Kwa kuongeza katika kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa, mpango unatarajiwa kuwa na faida kubwa katika kupunguza umaskini, hifadhi ya bayoanuwai na kupunguza makali ya madhara yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Utafiti wa kiuchumi uliofanywa na Wizara ya Kilimo, Maji na Uvuvi mwaka 2009 ulionyesha kuwa uwekezaji wa aina hii unaweza kuongeza mapato kwa wakulima kati ya asilimia 25 hadi 40.

Kwa mujibu wa Rasmane Ouédraogo, mratibu wa Mpango wa Kitaifa wa Umaskini na Mazingira, misitu ni muhimu kwa kipato cha wananchi wa Burkina Faso, ambapo asilimia 80 ya wakazi wanategemea rasilimali kuendeshea maisha yao. (END//2013)

Back to radio index >>

Republish | | Print |