Africa:
Kuhakikisha Wakulima Wadogo Wadogo wa Ghana Wanakabiliana na Hali ya Hewa

Reprint | | Print |

TAMALE, Ghana - Wakulima wadogo wadogo nchini Ghana wamevutiwa na kuanzishwa kwa mpango wa bima unaojulikana kama Mpango wa Bima ya Kilimo Ghana (GAIP) ambao utasaidia wakulima ambao wamepoteza kipato kutokana na hali mbaya ya hewa kuathiri mavuno.
 
Mtaalam wa Hali ya Hewa katika GAIP Evelyn Debrah anasema faida za mpango huo kwa wakulima ni kuwalinda kutokana na gharama za uzalishaji wakati wa hali mbaya ya hewa na kuwaruhusu kuendelea kuzalisha kufuatia janga hilo.

Mkulima hulipia moja ya kumi ya gharama zote za mazao yake kwa GAIP katika kipindi cha mwanzoni mwa msimu wa kilimo. Na kama kutakosekana mvua kwa siku 12 mfululizo, mfumo unaashiria mkulima kupatiwa malipo, kutegemeana na kiwango cha ardhi na kiasi cha pembejeo alizowekeza.

Mpango huo uko katika mwaka wake wa pili wa utekelezaji, na hadi sasa jumla ya wakulima wadogo wadogo 136 wameshapata malipo kutoka kwa GAIP kutokana na kutokea kwa ukame kaskazini mwa Ghana. (END//2013)

Back to radio index >>

Republish | | Print |