Africa:
Wakulima Wadogo Nchini Kenya Wakosa Uhakika wa Shughuli Yao

Reprint | | Print |

NAIROBI - Wakulima nchini Kenya na hasa wakulima wadogo wadogo wanakabiliwa na wakati mgumu wa kukosa mazao kutokana na hali mbaya ya hewa kwani chanzo hicho kikubwa cha maji nchini humo kinazalisha maji kidogo zaidi ikilinganishwa na siku za zamani.
 
Chai, moja ya zao linaloingizia nchi fedha nyingi za kigeni katika thamani ya dola bilioni 1.17, kwa mujibu wa Taasisi ya Takwimu ya Taifa, ni miongoni mwa mazao yaliyopo katika hatari kubwa. Wataalam wanakadiria kuwa mabadiliko ya tabia nchi yanaweza kugharimu wakulima wa chai hadi asilimia 30 ya mapato yao ya fedha.

Joel Nduati, mkulima mdogo mdogo katikati mwa Kenya, anasema kukosekana kwa taarifa za kuchukua hatua kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa limekuwa tatizo lao kubwa.

Kwa mujibu wa Gathuru Mburu, mratibu wa Mtandao wa Bayoanuwai Afrika, maarifa ya jadi yanaweza kuwa ufumbuzi kwa kuwa yanaleta harakati za kiikolojia na kilimo katika ngazi ya chini kabisa ya jamii. (END//2013)

Back to radio index >>

Republish | | Print |