UAE-SYRIA: Baraza la Biashara lazinduliwa mjini Damascus Kwa Wahariri: Taarifa ifuatayo imetolewa na Shirika la Habari la Falme za Kiarabu (WAM)
DAMASCUS, Des. 28 (WAM) - Baraza la Biashara la Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE) na Syria lilizinduliwa jana jioni mjini Damascus mbele ya Waziri wa Biashara za Nje wa UAE Sheikha Lubna bint Khalid Al Qasimim na Naibu Waziri Mkuu wa Syria anayehusika na Masuala ya Uchumi Abdullah Dardari.
Katika hotuba yake Sheikha Lubna alithibitisha kuwa UAE na Syria wana uhusiano wa karibu chini ya usimamizi wa uongozi wa busara wa nchi hizo mbili, akibainisha kuwa maendeleo yanayopatikana katika mahusiano yao na kuwasiliana kwa mara kwa mara kwa jumuiya za wafanyabiashara za nchi hizo mbili kumetafsiri matokeo ya miaka mingi ya kuwasiliana na mwingiliano na hivyo kuchangia kwa ujumla katika kukuza ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo ya biashara na uwekezaji.
Sheikha Lubna alitoa pongezi zake kwa kuzinduliwa kwa Baraza la Biashara la UAE na Syria, ambalo ni matokeo ya maendeleo ya mahusiano baina ya nchi hizo mbili, akisema kuwa jumuiya ya wafanyabiashara ni nguvu kuu inayosukuma biashara na mahusiano ya kiuchumi ya nchi hizo mbili. (WAM) (END/2010)
(END/2010)
|
|
|