INDIA-PAKISTAN: Waelekeza Nguvu Katika Kujenga Vitega Uchumi na Mitandao ya Kiuchumi, Linasema Gazeti la UAE Kwa Wahariri: Taarifa ifuatayo imetolewa na Shirika la Habari la Falme za Kiarabu (WAM)
ABU DHABI, Aprili 10 (WAM) - Gazeti katika Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE) limesema kuwa uboreshwaji wa mahusiano na mazungumzo ya mara kwa mara kati ya India na Pakistan kutaleta faida kwa nchi zote mbili na kutaondokana na masuala ambayo yamefanya mchakato huu kuwa adui kwa miaka mingi sasa.
Likizungumza kuhusu ziara ya Rais wa Pakistan Asif Ali Zardari nchini India, gazeti la Gulf News katika tahariri yake lilisema kuwa ziara hiyo imekuja kupongezwa na wakati huo huo kama matusi.
"Lakini ukweli unabakia kuwa ni ziara ya kwanza ya kiserikali iliyofanywa na mkuu wa nchi kutoka pande zote za nchi hizo kwa kipindi cha miaka saba. Na pamoja na kwamba pande zote mbili zilifanya kazi kwa muda mrefu kupunguza matarajio ya umma, Zardari na Waziri Mkuu Manmohan Singh walisema waliridhishwa na chanzo cha ziara hiyo."
Gazeti liliongeza: "Katika suala hilo, India na Pakistan inaonekana kuwa na nia ya kuweka pembeni masuala tata kwa wakati huu na kujikita katika kujenga vitega uchumi na mahusiano ya kibiashara." (WAM)
(END/2012)
|
|
|