UAE: Wizara ya Mambo ya Ndani Yaadhimisha Siku ya Kupambana na Ajira za Watoto Duniani Kwa Wahariri: Taarifa ifuatayo inaletwa kwenu na Shirika la Habari la Falme za Kiarabu (WAM)
ABU DHABI, Jun 13 (WAM) - Meja Jenerali Nasser Lakhraibani Al Nuaimi, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Waziri Mkuu, Waziri wa Mambo ya Ndani na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kulinda Haki za Watoto, imesisitiza kuwa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Ajira kwa Watoto Duniani (WDACL) Wizara ya Mambo ya Ndani ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) imejiandaa kikamilifu kusaidia jitihada za ndani na za kimataifa kulinda watoto kutokana na unyanyasaji wa kila aina.
Alisema kuwa wizara imejizatiti kuzingatia kanuni za kimataifa za kulinda haki za watoto na kusambaza ufahamu juu ya unyanyasaji wa watoto.
Al Nuaimi aliunga mkono jitihada za wizara tangu ilipojiunga na Kikundi Kazi cha Ubadilishanaji wa Taarifa wa Masafa ya Mbali Duniani (VGT) na kuanzisha Kamati Kuu, na Kituo cha Kulinda Haki za Watoto.
Aliongeza kuwa ajira kwa watoto inaacha madhara hasi kwa jamii kwa ujumla na hasa watoto.
Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Ajira kwa Watoto ni siku ya Shirika la Kazi la Kimataifa (ILO) kwa lengo la kuongeza ufahamu na uanaharakati kuzuia ajira kwa watoto katika nyanja za kiuchumi na kijeshi. Maadhimisho yanafanyika kila mwaka Juni 12. ILO ilianzisha siku hiyo mwaka 2002 na imekuwa ikiadhimishwa kila mwaka tangu wakati huo. (END/2012)
|
|
|