UAE: RCA Yapeleka Misaada ya Kiutu kwa Waathirika wa Ukame nchini Mauritania Kwa Wahariri: Taarifa ifuatayo inaletwa kwenu na Shirika la Habari la Falme za Kiarabu (WAM)
NOUAKCHOTT, Jun 26 (WAM) - Mamlaka ya Nusu Mwezi (RCA) ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa kushirikiana na Ubalozi wa UAE nchini Mauritania ilitoa misaada ya kiutu kwa wale walioathirika na ukame hapa. Ilihusu vifaa vya chakula, kama vile mchele, ngano, sukari na mafuta.
Hatua hiyo inakuja katika muktadha mzima wa RCA wa kukabiliana na madhara ya njaa na ukame katika Pwani ya Magharibi mwa Afrika.
Zaidi ya watu milioni 14 katika nchi kadhaa za Afrika Magharibi wameathirika na ukame ambao umesababisha kukosekana kwa usalama wa chakula na utapiamlo, hasa miongoni mwa watoto. Mauritania, Niger, Chad, Mali, Burkina Faso na baadhi ya mikoa nchini Senegal imeathirika vibaya na ukame ambao umeshawaua watu 300,000 katika kipindi cha mwaka mmoja.
(END/2012)
|
|
|