UAE: Timu ya Mpira wa Miguu ya Taifa Ina Mustakabali Bora wa Baadaye Kwa Wahariri: Taarifa ifuatayo imetolewa na Shirika la Habari la Falme za Kiarabu (WAM)
ABU DHABI, Julai 31 (WAM) - Mafanikio ya timu ya mpira wa miguu ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) katika Michezo ya Olimpiki yanafaa kupongezwa. Wachezaji walionyesha uwezo mkubwa bila kujali kuwa walipoteza mechi za kwanza katika ngazi ya makundi, limesema gazeti la ‘Gulf News’.
Gazeti hilo limesema katika tahariri yake ya leo: "Hii ni mara ya kwanza kwa timu ya UAE kushiriki katika mpira wa miguu kwenye Michezo ya Olimpiki. Huu ni uzoefu mpya na hivyo jinsi timu ilivyocheza inafaa kupongezwa na kutiwa hamasa zaidi. Hata hivyo, timu ya UAE ina wachezaji vijana zaidi ambao walicheza na wapinzani wao waliokuwa na wachezaji wenye majina makubwa na uzoefu wa kimataifa. Timu ilikabiliana na changamoto hii kubwa kwa kuonyesha weredi wa kiwango cha juu."
Timu ya UAE imeonyesha uwezo mkubwa wa uwezekano wa kufika mbali katika siku zijazo kutokana na mazao yake ya wachezaji wenye vipaji na shauku. Hakuna shaka timu ina mustakabali mzuri wa baadaye na kwa kupewa muda, mafunzo na matunzo, timu hii itabeba vizuri bendera ya nchi. Matokeo ya timu ya mpira wa miguu katika siku chache za karibuni yanatia moyo na kuna mambo mazuri zaidi ya kutarajiwa katika siku zijazo.
(END/2012)
|
|
|